Ezra 2
Orodha Ya Watu Waliorudi Kutoka Uhamishoni
(Nehemia 7:4-73)
1Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana):Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa:
3 ▼
4– 5– 6– 7– 8– 9– 10– 11– 12– 13– 14– 15– 16– 17– 18– 19– 20– ▼Ili kupanga jedwali lililo katika mstari huu kwa usahihi, imekuwa muhimu kuhamisha maudhui ya aya 4-Ezr 2:20 ndani yake.
| wazao wa Paroshi | 2,172 |
| (4) wazao wa Shefatia | 372 |
| (5) wazao wa Ara | 775 |
| (6) wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) | 2,812 |
| (7) wazao wa Elamu | 1,254 |
| (8) wazao wa Zatu | 945 |
| (9) wazao wa Zakai | 760 |
| (10) wazao wa Bani | 642 |
| (11) wazao wa Bebai | 623 |
| (12) wazao wa Azgadi | 1,222 |
| (13) wazao wa Adonikamu | 666 |
| (14) wazao wa Bigwai | 2,056 |
| (15) wazao wa Adini | 454 |
| (16) wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) | 98 |
| (17) wazao wa Besai | 323 |
| (18) wazao wa Yora | 112 |
| (19) wazao wa Hashumu | 223 |
| (20) wazao wa Gibari | 95 |
21 ▼
22– 23– 24– 25– 26– 27– 28– 29– 30– 31– 32– 33– 34– 35– ▼Ili kupanga jedwali lililo katika mstari huu kwa usahihi, imekuwa muhimu kuhamisha maudhui ya aya 22-Ezr 2:35 ndani yake.
| watu wa Bethlehemu | 123 |
| (22) watu wa Netofa | 56 |
| (23) watu wa Anathothi | 128 |
| (24) watu wa Azmawethi | 42 |
| (25) wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi | 743 |
| (26) wazao wa Rama na Geba | 621 |
| (27) watu wa Mikmashi | 122 |
| (28) watu wa Betheli na Ai | 223 |
| (29) wazao wa Nebo | 52 |
| (30) wazao wa Magbishi | 156 |
| (31) wazao wa Elamu ile ingine | 1,254 |
| (32) wazao wa Harimu | 320 |
| (33) wazao wa Lodi, Hadidi na Ono | 725 |
| (34) wazao wa Yeriko | 345 |
| (35) wazao wa Senaa | 3,630 |
36 ▼
37– 38– 39– 43Watumishi wa Hekalu: ▼▼Ili kupanga jedwali lililo katika mstari huu kwa usahihi, imekuwa muhimu kuhamisha maudhui ya aya 37-Ezr 2:39 ndani yake.
Makuhani:| wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) | 973 |
| (37) wazao wa Imeri | 1,052 |
| (38) wazao wa Pashuri | 1,247 |
| (39) wazao wa Harimu | 1,017 |
wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
44wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni,
45wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu,
46wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani,
47wazao wa Gideli, Gahari, Reaya,
48wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu,
49wazao wa Uza, Pasea, Besai,
50wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu,
51wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
52wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
53wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
54wazao wa Nesia na Hatifa.
55Wazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda,
56wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
57wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami.
59Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
61Kutoka miongoni mwa makuhani:
Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
62Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu. ▼
▼Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha kifuani cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.
64Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 65tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. 66Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, 67ngamia 435 na punda 6,720.
68Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 69Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 ▼
▼Darkoni 61,000 za dhahabu ni sawa na kilo 500.
za dhahabu, mane 5,000 ▼▼Mane 5,000 za fedha ni sawa na kilo 2,900.
za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo. 70Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.
Copyright information for
SwhNeno