Isaiah 38:1-3
Kuugua Kwa Mfalme Hezekia
(2 Wafalme 20:1-11; 2 Nyakati 32:24-26)
1Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.” 2Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana: 3“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.
Copyright information for
SwhNeno