‏ Joshua 12

Orodha Ya Wafalme Walioshindwa

1Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:

2Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.

Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
3Pia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi
Yaani Bahari ya Galilaya.
hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi
Yaani Bahari Mfu.
), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.

4Nayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

5Naye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

6Mose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

7Hawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao: 8nchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):

9
Ili kupanga jedwali lililo katika mstari huu kwa usahihi, imekuwa muhimu kuhamisha maudhui ya aya 10-Jos 12:23 ndani yake.
mfalme wa Yeriko mmoja
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja
(10) mfalme wa Yerusalemu mmoja
mfalme wa Hebroni mmoja
(11) mfalme wa Yarmuthi mmoja
mfalme wa Lakishi mmoja
(12) mfalme wa Egloni mmoja
mfalme wa Gezeri mmoja
(13) mfalme wa Debiri mmoja
mfalme wa Gederi mmoja
(14) mfalme wa Horma mmoja
mfalme wa Aradi mmoja
(15) mfalme wa Libna mmoja
mfalme wa Adulamu mmoja
(16) mfalme wa Makeda mmoja
mfalme wa Betheli mmoja
(17) mfalme wa Tapua mmoja
mfalme wa Heferi mmoja
(18) mfalme wa Afeki mmoja
mfalme wa Lasharoni mmoja
(19) mfalme wa Madoni mmoja
mfalme wa Hazori mmoja
(20) mfalme wa Shimron-Meroni mmoja
mfalme wa Akishafu mmoja
(21) mfalme wa Taanaki mmoja
mfalme wa Megido mmoja
(22) mfalme wa Kedeshi mmoja
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja
(23) mfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori)
Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori.
mmoja
mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja
(24) mfalme wa Tirsa mmoja

10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24

wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.
Copyright information for SwhNeno