‏ Luke 23:1-5

Yesu Apelekwa Kwa Pilato

(Mathayo 27:1-14; Marko 15:1-5; Yohana 18:28-38)

1Kisha umati wote wa watu ukainuka na kumpeleka Yesu kwa Pilato. 2Nao wakaanza kumshtaki wakisema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu, akiwazuia watu wasilipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo,
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
mfalme.”

3Basi Pilato akamuuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

Yesu akajibu, “Wewe wasema.”

4Pilato akawaambia viongozi wa makuhani na watu wote waliokuwepo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki mtu huyu!”

5Lakini wao wakakazana kusema, “Anawachochea watu kwa mafundisho yake katika Uyahudi yote, tangu Galilaya alikoanzia, hadi sehemu hii!”
Copyright information for SwhNeno