Luke 23:44-49
Kifo Cha Yesu
(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Yohana 19:28-30)
44Ilikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa, 45kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili. 46Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho. 47Yule jemadari alipoona yaliyotukia, akamsifu Mungu, akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48Watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao. 49Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wale wanawake waliokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyatazama mambo haya.
Copyright information for
SwhNeno