Luke 4:14-15
Mwanzo Wa Huduma Ya Galilaya
(Mathayo 4:12-17; Marko 1:14-15)
14Kisha Yesu akarudi mpaka Galilaya, akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, nazo habari zake zikaenea katika sehemu zote za nchi za kandokando. 15Akaanza kufundisha kwenye masinagogi yao, na kila mmoja akamsifu.
Copyright information for
SwhNeno