Mark 12:35-37
Kristo Ni Mwana Wa Nani?
(Mathayo 22:41-46; Luka 20:41-44)
35Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, akauliza, “Imekuwaje walimu wa sheria wanasema kwamba Kristo ▼▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
ni Mwana wa Daudi? 36Kwa maana Daudi mwenyewe, akinena kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, alisema: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’
37 Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?” Ule umati wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha.
Copyright information for
SwhNeno