‏ Mark 14:22-26

Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana

(Mathayo 26:26-30; Luka 22:14-20; 1 Wakorintho 11:23-25)

22Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.”

23Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo.

24Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. 25Amin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika Ufalme wa Mungu.”

26Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.
Copyright information for SwhNeno