Mark 14:27-31
Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana
(Mathayo 26:31-35; Luka 22:31-34; Yohana 13:36-38)
27Yesu akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: “ ‘Nitampiga mchungaji,nao kondoo watatawanyika.’
28 Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.” 29Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.” 30Yesu akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.” 31Lakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.
Copyright information for
SwhNeno