Mark 8:11-13
Mafarisayo Waomba Ishara
(Mathayo 12:38-42; 16:1-4)
11Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 12Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Amin nawaambieni, hakitapewa ishara yoyote.” 13Kisha akawaacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ngʼambo.
Copyright information for
SwhNeno