Matthew 13:53-58
Yesu Akataliwa Nazareti
(Marko 6:1-6; Luka 4:16-30)
53Yesu alipomaliza kutoa mifano hii, akaondoka. 54Alipofika mji wa kwao, akawafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza?” 55“Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si yeye aitwaye Maria, nao ndugu zake si Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56Nao dada zake wote, hawako hapa pamoja nasi? Mtu huyu amepata wapi basi mambo haya yote?” 57Wakachukizwa naye. Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani kwake.” 58Naye hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.
Copyright information for
SwhNeno