Matthew 18:1-5
Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni
(Marko 9:33-37; Luka 9:46-48)
1Wakati huo, wanafunzi wakamjia Yesu na kumuuliza, “Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni?” 2Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. 3Naye akasema: “Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. 4Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni. 5 “Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi.
Copyright information for
SwhNeno