Matthew 24:32-35
32 “Basi jifunzeni somo hili kutokana na mtini: Matawi yake yanapoanza kuchipua na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 33Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yote, mnatambua kwamba wakati u karibu, hata malangoni. 34Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 35Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Copyright information for
SwhNeno