Matthew 4:12-17
Yesu Aanza Kuhubiri
(Marko 1:14-15; Luka 4:14-15)
12Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya. 13Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na Naftali, 14ili kutimiza unabii wa nabii Isaya, kama alivyosema: 15“Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,kwenye njia ya kuelekea baharini,
ngʼambo ya Yordani,
Galilaya ya watu wa Mataifa:
16watu wale waliokaa gizani
wameona nuru kuu;
nao wale walioishi katika nchi ya uvuli wa mauti,
nuru imewazukia.”
17Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”
Copyright information for
SwhNeno