‏ Matthew 4:23-25

Yesu Ahubiri Na Kuponya Wagonjwa

(Luka 6:17-19)

23Yesu akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu. 24Kwa hiyo sifa zake zikaenea sehemu zote za Shamu, nao watu wakamletea wote waliokuwa na magonjwa mbalimbali na maumivu, waliopagawa na pepo wachafu, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya. 25Makutano makubwa ya watu yakawa yanamjia kutoka Galilaya, Dekapoli,
Yaani Miji Kumi.
Yerusalemu, Uyahudi na kutoka ngʼambo ya Mto Yordani.
Copyright information for SwhNeno