Matthew 8:14-17
Yesu Aponya Wengi
(Marko 1:29-34; Luka 4:38-41)
14Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa. 15Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia. 16Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. 17Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba: “Mwenyewe alitwaa udhaifu wetuna alichukua magonjwa yetu.”
Copyright information for
SwhNeno