‏ Nehemiah 7

1Baada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. 2Nikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. 3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”

Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni

(Ezra 2:1-70)

4Mji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. 5Hivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:

6Hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 7wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):

Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:
8
Ili kupanga jedwali lililo katika mstari huu kwa usahihi, imekuwa muhimu kuhamisha maudhui ya aya 9-Neh 7:25 ndani yake.
wazao wa Paroshi 2,172
(9) wazao wa Shefatia 372
(10) wazao wa Ara 652
(11) wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,818
(12) wazao wa Elamu 1,254
(13) wazao wa Zatu 845
(14) wazao wa Zakai 760
(15) wazao wa Binui 648
(16) wazao wa Bebai 628
(17) wazao wa Azgadi 2,322
(18) wazao wa Adonikamu 667
(19) wazao wa Bigwai 2,067
(20) wazao wa Adini 655
(21) wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98
(22) wazao wa Hashumu 328
(23) wazao wa Besai 324
(24) wazao wa Harifu 112
(25) wazao wa Gibeoni 95

9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25
26
Ili kupanga jedwali lililo katika mstari huu kwa usahihi, imekuwa muhimu kuhamisha maudhui ya aya 27-Neh 7:38 ndani yake.
watu wa Bethlehemu na Netofa 188
(27) watu wa Anathothi 128
(28) watu wa Beth-Azmawethi 42
(29) watu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743
(30) watu wa Rama na Geba 621
(31) watu wa Mikmashi 122
(32) watu wa Betheli na Ai 123
(33) watu wa Nebo 52
(34) wazao wa Elamu 1,254
(35) wazao wa Harimu 320
(36) wazao wa Yeriko 345
(37) wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 721
(38) wazao wa Senaa 3,930

27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38
39
Ili kupanga jedwali lililo katika mstari huu kwa usahihi, imekuwa muhimu kuhamisha maudhui ya aya 40-Neh 7:42 ndani yake.
Makuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973
(40) wazao wa Imeri 1,052
(41) wazao wa Pashuri 1,247
(42) wazao wa Harimu 1,017

40 41 42
43Walawi:

wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia)     74

44Waimbaji:

wazao wa Asafu     148

45Mabawabu wa malango:

wazao wa

Shalumu, Ateri, Talmoni,

Akubu, Hatita na Shobai    
138

46Watumishi wa Hekalu:
Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).

wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
47wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,
48wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,
49wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,
50wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,
51wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,
52wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,
53wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
55wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
56wazao wa Nesia na Hatifa.

57Wazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,
58wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
59wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.
60
Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392

61Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
62
wazao wa

Delaya, Tobia na Nekoda
642

63Na kutoka miongoni mwa makuhani:
wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
64Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 65Kwa hiyo, mtawala
Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70).
aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.
Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.

66Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245. 68Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245 69ngamia 435 na punda 6,720.

70Baadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000
Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6.
za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.
71Baadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu,
Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172.
na mane 2,200
Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300.
za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

72Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.

73Makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.

Ezra Asoma Sheria

Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,
Copyright information for SwhNeno