‏ Psalms 120

Kuomba Msaada

Wimbo wa kwenda juu.

1Katika dhiki yangu namwita Bwana,
naye hunijibu.
2Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo
na ndimi za udanganyifu.

3Atakufanyia nini,
au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,
kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.

5Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,
kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!
6Nimeishi muda mrefu mno
miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7Mimi ni mtu wa amani;
lakini ninaposema, wao wanataka vita.
Copyright information for SwhNeno