Psalms 60:5-12
5Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,ili wale uwapendao wapate kuokolewa.
6Mungu amenena kutoka patakatifu pake:
“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi
na kulipima Bonde la Sukothi.
7Gileadi ni yangu na Manase ni yangu;
Efraimu ni kofia yangu ya chuma,
nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.
8Moabu ni sinia langu la kunawia,
juu ya Edomu natupa kiatu changu;
nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”
9Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?
Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?
10Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,
na hutoki tena na majeshi yetu?
11Tuletee msaada dhidi ya adui,
kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.
12Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,
naye atawaponda adui zetu.
Copyright information for
SwhNeno