‏ Psalms 87

Sifa Za Yerusalemu

Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo.

1Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu;
2 Bwana anayapenda malango ya Sayuni
kuliko makao yote ya Yakobo.
3Mambo matukufu yanasemwa juu yako,
ee mji wa Mungu:
4“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu
Rahabu hapa ni jina la ushairi la Misri.
na Babeli
miongoni mwa wale wanaonikubali mimi:
Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi,
Kushi hapa ina maana ya Naili ya juu, yaani Ethiopia.

nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ”

5Kuhusu Sayuni itasemwa hivi,
“Huyu na yule walizaliwa humo,
naye Aliye Juu Sana mwenyewe
atamwimarisha.”
6 Bwana ataandika katika orodha ya mataifa:
“Huyu alizaliwa Sayuni.”
7Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba,
“Chemchemi zangu zote ziko kwako.”
Copyright information for SwhNeno