Psalms 1
KITABU CHA KWANZA
(Zaburi 1–41)
Furaha Ya Kweli
1Heri mtu yule ambayehaendi katika shauri la watu waovu,
wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,
au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
2Bali huifurahia sheria ya Bwana,
naye huitafakari hiyo sheria usiku na mchana.
3Mtu huyo ni kama mti uliopandwa
kando ya vijito vya maji,
ambao huzaa matunda kwa majira yake
na majani yake hayanyauki.
Lolote afanyalo hufanikiwa.
Huzuni Ya Waovu
4Sivyo walivyo waovu!Wao ni kama makapi
yapeperushwayo na upepo.
5Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,
wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
6Kwa maana Bwana huziangalia njia za mwenye haki,
bali njia ya waovu itaangamia.
Copyright information for
SwhNeno