‏ Psalms 100

Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu

Zaburi ya shukrani.

1Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.
2Mwabuduni Bwana kwa furaha;
njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
3Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu.
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.

4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
5Kwa maana Bwana ni mwema
na upendo wake wadumu milele;
uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.
Copyright information for SwhNeno