Psalms 110
Bwana Na Mfalme Wake Mteule
Zaburi ya Daudi. 1 Bwana amwambia Bwana wangu:“Keti mkono wangu wa kuume,
mpaka nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
3Askari wako watajitolea kwa hiari
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako. ▼
▼Au: vijana wako watakujia kama umande.
4 Bwana ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
5Bwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7Atakunywa maji katika kijito kando ya njia, ▼
▼Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.
kwa hiyo atainua kichwa chake juu.
Copyright information for
SwhNeno