‏ Psalms 117

Sifa Za Bwana

1Msifuni Bwana, enyi mataifa yote;
mtukuzeni yeye, enyi watu wote.
2Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,
uaminifu wa Bwana unadumu milele.

Msifuni Bwana.
Copyright information for SwhNeno