‏ Psalms 121

Bwana Mlinzi Wetu

Wimbo wa kwenda juu.

1Nayainua macho yangu nitazame vilima,
msaada wangu utatoka wapi?
2Msaada wangu hutoka kwa Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia.

3Hatauacha mguu wako uteleze,
yeye akulindaye hatasinzia,
4hakika, yeye alindaye Israeli
hatasinzia wala hatalala usingizi.
5 Bwana anakulinda,
Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,
6jua halitakudhuru mchana,
wala mwezi wakati wa usiku.
7 Bwana atakukinga na madhara yote,
atayalinda maisha yako,
8 Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka,
tangu sasa na hata milele.
Copyright information for SwhNeno