‏ Psalms 70

Kuomba Msaada

(Zaburi 40:13-17)

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.

1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
2Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
3Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4Lakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Mungu na atukuzwe!”

5Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
Ee Bwana, usikawie.
Copyright information for SwhNeno