‏ Psalms 93

Mungu Mfalme

1 Bwana anatawala, amejivika utukufu;
Bwana amejivika utukufu
tena amejivika nguvu.
Dunia imewekwa imara,
haitaondoshwa.
2Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani;
wewe umekuwako tangu milele.

3Bahari zimeinua, Ee Bwana,
bahari zimeinua sauti zake;
bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.
4Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
Bwana aishiye juu sana ni mkuu.

5Ee Bwana, sheria zako ni imara;
utakatifu umepamba nyumba yako
pasipo mwisho.
Copyright information for SwhNeno