‏ 1 Chronicles 16:8-22

8Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
9Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa;
waambieni matendo yake yote ya ajabu.
10Lishangilieni jina lake takatifu;
mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
11Mtafuteni Bwana na nguvu zake;
utafuteni uso wake siku zote.
12Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,
miujiza yake na hukumu alizozitamka,
13enyi wazao wa Israeli mtumishi wake,
enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

14Yeye ndiye Bwana Mungu wetu;
hukumu zake zimo duniani pote.
15Hulikumbuka agano lake milele,
neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
16agano alilolifanya na Abrahamu,
kiapo alichomwapia Isaki.
17Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,
kwa Israeli liwe agano la milele:
18“Nitakupa wewe nchi ya Kanaani
kuwa sehemu utakayoirithi.”

19Walipokuwa wachache kwa idadi,
wachache sana na wageni ndani yake,
20walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,
kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
21Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;
kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
22“Msiwaguse niliowatia mafuta;
msiwadhuru manabii wangu.”
Copyright information for SwhNeno