2 Chronicles 9:29-31
Kifo Cha Solomoni
(1 Wafalme 11:41-43)
29Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Solomoni, kuanzia mwanzo hadi mwisho, je, hayakuandikwa katika kumbukumbu za nabii Nathani, katika unabii wa Ahiya Mshiloni na katika maono ya Ido mwonaji kuhusu Yeroboamu mwana wa Nebati? 30Solomoni alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu. 31Kisha Solomoni akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Copyright information for
SwhNeno