‏ 2 Kings 22:1-2

Yosia Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 34; 35:20-27)

1Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. Mama yake aliitwa Yedida binti Adaya, kutoka Boskathi. 2Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana na kuenenda katika njia zote za Daudi baba yake. Hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.
Copyright information for SwhNeno