2 Samuel 5:17-25
Daudi Awashinda Wafilisti
(1 Nyakati 14:8-17)
17Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome. 18Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, 19kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” Bwana akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.” 20Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu. ▼▼Maana yake Bwana Afurikae.
21Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua. 22Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. 23Kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, naye akamjibu, “Usipande moja kwa moja, bali wazungukie kwa nyuma na uwashambulie mbele ya miti ya miforosadi. 24Mara utakaposikia sauti ya kutembea kutoka kwenye vilele vya miti ya miforosadi, nenda haraka, kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa Bwana ametangulia mbele yako kupiga jeshi la Wafilisti.” 25Basi Daudi akafanya kama Bwana alivyomwagiza, naye akawaangusha Wafilisti njia yote kuanzia Geba ▼▼Kwa Kiebrania mji huu uliitwa Gibeoni (ona 1Nya 14:16).
hadi Gezeri.
Copyright information for
SwhNeno