‏ Exodus 25:1-9

Sadaka Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu

(Kutoka 35:4-9)

1 Bwana akamwambia Mose, 2“Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa niaba yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa. 3Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: dhahabu, fedha na shaba; 4nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; singa za mbuzi; 5ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;
Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.
mbao za mshita;
6mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; 7na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.

8“Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. 9Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha.
Copyright information for SwhNeno