‏ Genesis 36:1-19

Wazao Wa Esau

(1 Nyakati 1:34-42)

1Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu).

2Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi, 3pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi.

4Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli, 5Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani.

6Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake. 7Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao. 8Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri.

9Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri.

10Haya ndiyo majina ya wana wa Esau:
Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia.
11Wana wa Elifazi ni:
Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.
12Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau.
13Wana wa Reueli ni:
Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau.
14Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni:
Yeushi, Yalamu na Kora.

15Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau: Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni:
Temani, Omari, Sefo, Kenazi,
16Kora, Gatamu na Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Ada.
17Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni:
Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau.
18Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni:
Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana.

19Hawa ndio waliokuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hawa ndio waliokuwa wakuu wao.
Copyright information for SwhNeno