Genesis 36:20-30
20Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 21Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.22Wana wa Lotani walikuwa:
Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.
23Wana wa Shobali walikuwa:
Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
24Wana wa Sibeoni walikuwa:
Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.
25Watoto wa Ana walikuwa:
Dishoni na Oholibama binti wa Ana.
26Wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
27Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
28Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.
29Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 30Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.
Copyright information for
SwhNeno