Jeremiah 52:1-3
Anguko La Yerusalemu
(2 Wafalme 24:18–25:30)
1Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja. Jina la mama yake aliitwa Hamutali binti Yeremia, kutoka Libna. 2Alifanya maovu machoni pa Bwana, kama alivyofanya Yehoyakimu. 3Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira ya Bwana haya yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, naye mwishoni akawaondoa mbele zake. Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
Copyright information for
SwhNeno