John 1:19-28
Ushuhuda Wa Yohana Mbatizaji
(Mathayo 3:1-12; Marko 1:1-8; Luka 3:1-18)
19Huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Wayahudi walipowatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?” 20Yohana alikiri waziwazi pasipo kuficha akasema, “Mimi si Kristo.” ▼▼Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
21Wakamuuliza, “Wewe ni nani basi? Je, wewe ni Eliya?” Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.” “Je, wewe ni yule Nabii?” Akajibu, “Hapana.” 22Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?” 23Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Bwana.’ ” 24Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo 25wakamuuliza, “Kama wewe si Kristo, wala si Eliya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?” 26Yohana akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, ▼▼Hapa tafsiri zingine zinasema ndani ya maji.
lakini katikati yenu yupo mtu msiyemjua. 27Yeye ajaye baada yangu, sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.” 28Mambo haya yote yalitukia huko Bethania, ngʼambo ya Mto Yordani, mahali Yohana alipokuwa akibatiza.
Copyright information for
SwhNeno