‏ John 12:1-8

Maria Ampaka Yesu Mafuta Huko Bethania

(Mathayo 26:6-13; Marko 14:3-9)

1Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alikwenda Bethania mahali ambako Lazaro aliyekuwa amefufuliwa na Yesu alikuwa anaishi. 2Wakaandaa karamu kwa heshima ya Yesu. Martha akawahudumia wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Yesu. 3Kisha Maria akachukua chupa ya painti moja
Painti moja ni kama nusu lita.
yenye manukato ya nardo
Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri.
safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Yesu na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

4Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Yesu, akasema, 5“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300
Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300.
na fedha hizo wakapewa maskini?”
6Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

7Yesu akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. 8Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”
Copyright information for SwhNeno