John 6:15-21
15Yesu akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake.Yesu Atembea Juu Ya Maji
(Mathayo 14:22-33; Marko 6:45-52)
16Ilipofika jioni, wanafunzi wake waliteremka kwenda baharini. 17Wakaingia kwenye mashua, wakaanza kuvuka bahari kwenda Kapernaumu. Wakati huu kulikuwa tayari giza na Yesu alikuwa hajajumuika nao. 18Bahari ikachafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma. 19Wanafunzi walipokuwa wamekwenda mwendo wa karibu maili tatu au nne, ▼▼Maili tatu au nne ni kama kilomita 5 au 6.
walimwona Yesu akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana. 20Lakini Yesu akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.” 21Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.
Copyright information for
SwhNeno