Luke 18:35-43
Yesu Amponya Kipofu Karibu Na Yeriko
(Mathayo 20:29-34; Marko 10:46-52)
35Yesu alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. 36Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita, akauliza, “Kuna nini?” 37Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.” 38Akapaza sauti, akasema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!” 39Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!” 40Yesu akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza, 41“Unataka nikufanyie nini?” Akajibu, “Bwana, nataka kuona.” 42Yesu akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.” 43Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.
Copyright information for
SwhNeno