‏ Luke 20:41-44

Kristo Ni Mwana Wa Nani?

(Mathayo 22:41-46; Marko 12:35-37)

41Kisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristo
Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta.
ni Mwana wa Daudi?
42Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
43 hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako.” ’

44 Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”
Copyright information for SwhNeno