Luke 21:29-33
29Akawaambia mfano huu: “Uangalieni mtini na miti mingine yote. 30Inapochipua majani, ninyi wenyewe mnaweza kuona na kutambua wenyewe ya kuwa wakati wa kiangazi umekaribia. 31Vivyo hivyo, myaonapo mambo haya yakitukia, mnatambua kwamba Ufalme wa Mungu umekaribia. 32 “Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hadi mambo haya yote yawe yametimia. 33Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Copyright information for
SwhNeno