Luke 22:14-20
Kuanzishwa Kwa Meza Ya Bwana
(Mathayo 26:31-35; Marko 14:27-31; Yohana 13:36-38)
14Wakati ulipowadia, Yesu akaketi mezani pamoja na wale mitume wake. 15Kisha akawaambia, “Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16Kwa maana, nawaambia, sitaila tena Pasaka mpaka itakapotimizwa katika Ufalme wa Mungu.” 17Akiisha kukichukua kikombe, akashukuru, akasema, “Chukueni hiki mnywe wote. 18Kwa maana nawaambia tangu sasa sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.” 19Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 20Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, imwagikayo kwa ajili yenu.
Copyright information for
SwhNeno