‏ Luke 24:50-53

Kupaa Kwa Yesu Mbinguni

(Marko 16:19-20; Matendo 1:9-11)

50Akiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. 51Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. 52Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. 53Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen.
Copyright information for SwhNeno