Luke 9:1-6
Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili
(Mathayo 10:5-15; Marko 6:7-13)
1Yesu kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 2kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 3Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada. 4Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 5Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” 6Hivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.
Copyright information for
SwhNeno