Mark 10:1-12
Mafundisho Kuhusu Talaka
(Mathayo 19:1-12; Luka 16:18)
1Yesu akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukaenda kwake tena, naye kama ilivyokuwa desturi yake, akawafundisha. 2Baadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumuuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?” 3Yesu akawajibu, “Je, Mose aliwaamuru nini?” 4Wakajibu, “Mose aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.” 5Yesu akawaambia, “Mose aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 6Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. 7Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.’ 8Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja. 9Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.” 10Walipokuwa tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza kuhusu jambo hili. 11Akawajibu, “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine, anazini naye. 12Naye mwanamke amwachaye mumewe na kuolewa na mume mwingine, anazini.”
Copyright information for
SwhNeno