Mark 6:45-52
Yesu Atembea Juu Ya Maji
(Mathayo 14:22-33; Yohana 6:15-21)
45Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 46Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba. 47Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Yesu alikuwa peke yake katika nchi kavu. 48Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, 50kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!” 51Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa, 52kwa kuwa walikuwa hawajaelewa kuhusu ile mikate. Mioyo yao ilikuwa migumu.
Copyright information for
SwhNeno