‏ Matthew 20:29-34

Yesu Awaponya Vipofu Wawili

(Marko 10:46-52; Luka 18:35-43)

29Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu ulimfuata. 30Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”

31Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie.”

32Yesu akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”

33Wakamjibu, “Bwana, tunataka kuona.”

34Yesu akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.
Copyright information for SwhNeno