Matthew 21:1-11
Yesu Anaingia Yerusalemu Kwa Shangwe
(Marko 11:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19)
1Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, 2akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtamkuta punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee. 3Kama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.” 4Haya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema: 5“Mwambieni Binti Sayuni,‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako,
ni mnyenyekevu, naye amepanda punda,
juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ”
6Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyokuwa amewaagiza. 7Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake. 8Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani. 9Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema, “Hosana, ▼
▼Kiebrania kusema Okoa, basi likawa neno la shangwe.
Mwana wa Daudi!”“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”
“Hosana juu mbinguni!”
10Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” 11Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”
Copyright information for
SwhNeno