Matthew 21:12-17
Yesu Atakasa Hekalu
(Marko 11:15-19; Luka 19:45-48; Yohana 2:13-22)
12Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 13Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.” 14Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya. 15Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika. 16Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyaoumeamuru sifa’?”
17Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko.
Copyright information for
SwhNeno