‏ Matthew 22:34-40

Amri Kuu Kuliko Zote

(Marko 12:28-34; Luka 10:25-28)

34Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazisha Masadukayo, Mafarisayo wakakusanyika pamoja. 35Mmoja wao, mtaalamu wa sheria, akamuuliza swali ili kumjaribu, akisema, 36“Mwalimu, ni amri ipi katika Sheria iliyo kuu kuliko zote?”

37Yesu akamjibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39Nayo ya pili ni kama hiyo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40Amri hizi mbili ndizo msingi wa Sheria na Manabii.”
Copyright information for SwhNeno